SHEMEJI
NINA JAMBO
Akiwa
amejawa na kasumba,
Mwanagenzi
Mkenya kasakata Rumba,
Na
Kijana asiye wa hii Nyumba,
Matokeo
ni kutungwa Mimba,
Mimba
ambayo ilipo vimba, iliwaletea wanaKenya Simba,
Ndiposa
tukapata Mkhwasi!
Ati
naskia wee Ni raisi Ughaibuni,
Tena
ulianza na udiwani,
Je,
ni ukweli ama tu ni utani?
Ufalme
wako wavutia kama samaku, kutoka uvuo hadi Ukambani,
wanukia
kama karafuu, na sasa uwaja nyumbani
Mkhwasi,
karibu tena nyumbani
Rais
Obama, nina mawili matatu yakukueleza,
Kwanza,
Msichana wako Malia ana demandi,
Kutoka
kwa wa Maasai hadi kwa wa Nandi,
Eeeeeiiish,
ata mimi khandi,
Naona
kama anaweza nipa Shitandi,
Sura
yake mzuri mama, mpaka afanya nikose appetite !
Lakini
si ya Ugali wala kuku, mbali niya vipusa wengine!
Jambo
la pili Shemeji wa Ulaya,
Rais
wa Kenya akatueka haya,
Akafungueoko
kiwanda cha miwa cha Mumias,
Kumbe
nia yake ni kumaliza kanyuaji,
Ati
Busaa na Chang’aa sio uji,
Mbali
ni Vinywaji vinazoleta mauaji
Ndiposa
bwana shemeji,
Usikuje
mkono mtupu kama shikongoyoko
Angalau
beba sahani, kama mtoto wa Nerea
Eh
mwana weru Obama,
Uli
mtoto wa Mama,
Kutoka
nchi ya Kenya,
County
hiyo ya Ugenya
Ndiposa
nakuuliza swali,
Je,
wewe ni Gor ama Chui?
Basi
kama haujui,
Ingwe
ndio Chui,
Timu
isiyo na uadui,
Timu
ya Baba na Mama
Timu
ya kujivunia,
Timu
ishangazayo dunia,
Iletee
mipira na gunia,
AFC
timu ya dunia
Shemeji
nalikunja jamvi,
Lakini
la muhumi nishasema,
Mate
hapa jijini usije katema,
Ama
Kidero akurudishe mapema, kwa kukiuka sharia za jiji
Lakini
usisahau, pia kakamega ni Mji,
Unaweza
pitia unywe chai Alhamisi,
Ndio
Ijumaa ukamuone Raisi,
Karibu
Rais Obama,
Kwa
nchi ya Baba na Mama!
By, Vincent Murimi
@vinniewatz
No comments:
Post a Comment