BAKE Tracker

Monday 27 July 2015

SHEMEJI NINA JAMBO
Akiwa amejawa na kasumba,
Mwanagenzi Mkenya kasakata Rumba,
Na Kijana asiye wa hii Nyumba,
Matokeo ni kutungwa Mimba,
Mimba ambayo ilipo vimba, iliwaletea wanaKenya Simba,
Ndiposa tukapata Mkhwasi!

Ati naskia wee Ni raisi Ughaibuni,
Tena ulianza na udiwani,
Je, ni ukweli ama tu ni utani?
Ufalme wako wavutia kama samaku, kutoka uvuo hadi Ukambani,
wanukia kama karafuu, na sasa uwaja nyumbani
Mkhwasi, karibu tena nyumbani


Rais Obama, nina mawili matatu yakukueleza,
Kwanza, Msichana wako Malia ana demandi,
Kutoka kwa wa Maasai hadi kwa wa Nandi,
Eeeeeiiish, ata mimi khandi,
Naona kama anaweza nipa Shitandi,
Sura yake mzuri mama, mpaka afanya nikose appetite !
Lakini si ya Ugali wala kuku, mbali niya vipusa wengine!

Jambo la pili Shemeji wa Ulaya,
Rais wa Kenya akatueka haya,
Akafungueoko kiwanda cha miwa cha Mumias,
Kumbe nia yake ni kumaliza kanyuaji,
Ati Busaa na Chang’aa sio uji,
Mbali ni Vinywaji vinazoleta mauaji
Ndiposa bwana shemeji,
Usikuje mkono mtupu kama shikongoyoko
Angalau beba sahani, kama mtoto wa Nerea

Eh mwana weru Obama,
Uli mtoto wa Mama,
Kutoka nchi ya Kenya,
County hiyo ya Ugenya
Ndiposa nakuuliza swali,
Je, wewe ni Gor ama Chui?
Basi kama haujui,
Ingwe ndio Chui,
Timu isiyo na uadui,
Timu ya Baba na Mama
Timu ya kujivunia,
Timu ishangazayo dunia,
Iletee mipira na gunia,
AFC timu ya dunia

Shemeji nalikunja jamvi,
Lakini la muhumi nishasema,
Mate hapa jijini usije katema,
Ama Kidero akurudishe mapema, kwa kukiuka sharia za jiji
Lakini usisahau, pia kakamega ni Mji,
Unaweza pitia unywe chai Alhamisi,
Ndio Ijumaa ukamuone Raisi,
Karibu Rais Obama,
Kwa nchi ya Baba na Mama!

By, Vincent Murimi
@vinniewatz 

No comments:

Post a Comment